BAHRAIN
Muandamanaji wa kishia auwawa na polisi nchini Bahrain
Polisi nchini Bahrain wamemuua muandamanaji mmoja wa kishia baada ya kurusha mabomu ya machozi kujaribu kuwatawanya waandamanaji wapinzani nchini humo wameeleza
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Taarifa zaidi kutoka kundi la upinzani la washia zinasema kuwa muandamanaji huyo Sayyed Hashem Saeed,mwenye umri wa miaka 15, alipigwa na bomu kichwani na mtu aliyejaribu kumsaidia alijeruhiwa eneo la paja.
Wakati huohuo mkuu mpya wa polisi aliyeteuliwa hivi karibuni amesema kuwa askari wapatao mia tano watasambazwa nchi nzima ikiwa ni pamoja na washia kusaidia kukuza mahusiano ya jamii wakati nchi inajaribu kujifunza kutokana na machafuko yaliyopita.