Pata taarifa kuu
Korea Kusini-Mazishi

Maelfu ya wananchi wa Korea Kaskazini washuhudia shughuli za mazishi ya kiongozi wao Kim Jong III

Maelfu ya wananchi wa korea Kaskazini hivi sasa wanshuhudia mazishi ya kiongozi wa tifa hilo Kim Jong Ill ambaye mwili wake utahifadhiwa katika jumba la kumbukumbu la nchi hiyo mjini Pyongyang.

shughuli za mazishi ya kiongozi wa Korea Kaskazini
shughuli za mazishi ya kiongozi wa Korea Kaskazini
Matangazo ya kibiashara

Televisheni ya taifa ya korea kaskazini imeonesha maelfu ya wanajeshi na raia wakiwa wameinamisha vichwa chini katika eneo la jumba la makumbusho ya taifa ambako mazishi hayo yanafanyakia wakitoa heshima zao za mwsho.

Mtoto wa Kim Jong Ill, Kim Jon Un ameonekana akiwa mstari wa mbele jirani na gari lililoubeba mwili wa baba yake akiambata na maofisa wengine wa juu wa jeshi la nchi hiyo kuelekea eneo la maziko.

Huku barafu kubwa ikiwa imetanda katika eneo hilo bado maelfu ya raia wameendelea kujitokeza kwa uwingi kushuhudia mazishi hayo ambayo yameelezwa kuwa yakihistoria ukilinganisha na yale ya mazishi ya baba yake.

Kim Jong Ill alifariki dunia juma moja lililopita kwa mshtuko wa moyo ambapo kabla ya kifo chake alimtangaza mtoto wake Kim Jong Un kama mrithi wa nafasi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.