Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Hofu ya uongozi yatanda Korea kaskazini siku mbili kabla ya maziko ya Kim Jong Il.

Wakati wananchi wa Korea Kaskazini wakitarajiwa kumzika kiongozi wao Kim Jong Il siku ya Jumatano, matiafa ya magharibi yameendelea kufuatilia kwa ukaribu hali ya kisiasa inavyoendelea nchini humo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Il wakati wa uhai wake
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Il wakati wa uhai wake AFP
Matangazo ya kibiashara

Wasiwasi kuhusu mustakabali wa taifa hilo unakuja wakati ambapo tayari chama cha wafanyakazi nchini humo kimemtangaza mtoto wa kim Jong il, Kim Jong Un kuwa kiongozi moyo wa taifa hilo akichukua nafasi ya baba yake.

Mbali na mtoto huyo kuteuliwa kushika uongozi wa taifa hilo, pia shemeji yake Jang Song Thaek na dada yake Kim Yong Hui wanaelezwa kushikilia nafasi za juu kwenye chama na jeshi hali inayozua hofu kuhusu uongozi wao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.