Ulaya
Nick Clegg amshambulia Cameron
Naibu waziri mkuu nchini uingereza Nick Clegg amemshambulia waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameron kufuatia kuitenga uingereza katika umoja wa ulaya kwa kura ya turufu ya mabadiliko ya mkataba wa EU.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Vyanzo vya karibu na kiongozi huyo wa Liberal Democrat kilisema Nick Clegg haoni kushindikana kwa mazungumzo juu ya mgogoro wa eurozone jambo ambalo lingesababisha ufanisi katika mpango wa Uingereza.
Awali waziri Nick Clegg alisema serikali ya umoja ilikuwa imeungana katika msimamo wake lakini vyanzo vya karibu naye vimethibitisha kwamba serikali haifikirii kama jambo hilo ni mpango mzuri kwa uingereza.