Pata taarifa kuu
MISRI

Maelfu ya waandamanaji waendelea kujitokeza katika uwanja wa Tahrir.

Maelfu ya waandamanaji wameendelea kujitokeza katika viwanja vya Tahrir mjini Cairo nchini Misri, kupinga kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika siku ya jumatatu sambamba na kupinga uteuzi wa waziri mkuu wa zamani Kamal Al Ganzuri kuiongoza nchi hiyo.

Maelfu ya waandamanaji nchini Misri wakiwa kwenye uwanja wa Tahrir mjini Cairo
Maelfu ya waandamanaji nchini Misri wakiwa kwenye uwanja wa Tahrir mjini Cairo REUTERS/Mohamed Abd El-Ghany
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia kupitia televisheni ya taifa baada ya uteuzi huo Kamal amesema kuwa yupo tayari kuunda serikali mpya na kurejesha usalama na amani katika nchi hiyo.

Aidha baraza la serikali ya kijeshi ya nchi hiyo linaloongozwa na aliyekuwa waziri wa ulinzi katika serikali ya Hosni Mubarak Hussein Tantawi,limeahidi kukabidhi madaraka kwa rais atakaye chaguliwa mwezi June mwaka 2012.

Tayari watu arobaini na mmoja wamepoteza maisha tangu kuanza kwa maandamano hayo juma lililopita kupinga utawala wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.