Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN latangaza kusitisha operesheni ya Majeshi ya NATO nchini Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kwa kauli moja limepiga kura ya kumaliza Mamlaka ya Majeshi ya Kimataifa yaliyokuwa yanaongozwa na Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO operesheni zake nchini Libya baada ya kufanikisha kuangushwa kwa Utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.

DR
Matangazo ya kibiashara

Wanachama kumi na watano kwa kauli moja wametamatisha operesheni hiyo iliyoanza mwezi Marchi mwaka huu ikiwa na baraka za Azimio la Umoja wa Mataifa UN namba 1973 ambalo lilikuwa linayataka majeshi hayo kulinda anga lisitumike kufanya mashambulizi.

Baraza hilo la Umoja wa Mataifa UN limesema linasitisha operesheni hiyo kwa kutumia azimio namba 2016 ambalo linayataka majeshi ya NATO ifikapo tarehe 31 ya mwezi Oktoba kuondoka kabisa nchini Libya ya kuacha utawala mpya uendelea kuongoza.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN limesema litatumia njia nyingine kuweza kuusaidia Utawala wa Baraza la Mpito la Taifa NTC ambalo liliomba majeshi yao yaendelee kusalia hadi mwisho wa mwake 2011.

Kiongozi wa Libya Mustafa Abdel Jalil kwenye mkutano wa huko Doha nchini Qatar alinukuliwa akiomba huruma ya Majeshi ya NATO kuendelea kushika doria kwani bado kuna tishio kwa wale wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi kushambulia serikali.

Azimio hilo jipya ambalo limepitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN linaama kwa sasa limeondoa ruhusa ya Majeshi ya NATO kuendelea kulinda raia kama ambavyo waliruhusiwa kuanzia mwezi March mwaka huu kupitia azimio namba 1973.

Maamuzi ya kulinda anga la Libya yalipitishwa mwezi Februari na kisha kuanza kutekelezwa mwezi Machi lakini baadaye Urusi, China, Brazil, India na Afrika Kusini walikosa NATO ilivyotumia vibaya azimio hilo.

Majeshi ya ushirika kutoka Ufaransa, Uingereza na Marekani chini ya mwamvuli wa NATO yalionekana kuamua kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafanikisha kuangushwa kwa Utawala wa Kanali Gaddafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.