Pata taarifa kuu
Libya-Syrte

Waasi wa Libya wajiandaa kuishambulia Syrte na Bani Walid baada ya muda uliotolewa kumalizika

Muda wa mwisho uliokuwa umetolewa na serikali ya Baraza la mpito nchini Libya kwa aliekuwa rais wa nchi hiyo, Kanali Muamar Gaddafi na wafuasi wake kujisalimisha, ulimalizika tangu Septemba 9, 2011 usiku wa manane. Lakini mapigano yalianza tena masaa kadhaa kabla ya kujuwa matokeo ya mazungumzo. Muda huo wa siku 10 ulitolewa kwa wafuasi wa Gaddafi kujisalimisha kabla ya kuvamia mji wa Syrte na Bani Walid. Waasi watangaza kuanzisha mashambulizi.

Bani Walid, Septemba 9,2011. Wanaume wanaojitolea kupambana na vikosi vya Gaddafi.
Bani Walid, Septemba 9,2011. Wanaume wanaojitolea kupambana na vikosi vya Gaddafi. © Reuters/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Milio ya roketi, na zana nzitonzito iemaza kusikika, inaashiria kwamba muda wa mazungumzo umekwisha.

Baada ya siku kumi za kusubiri kuivamia miji ya Sirte na Bani Walid, wapiganaji wa baraza la mpito walivamiwa kwa kushtukizwa na mizinga ya wafuasi wa kanali Gaddafi bila kutarajiwa.

Wanajeshi tiifu kwa kanalai Muamar Gaddafi walianzisha mapigano na kuonyesha kwamba bado wana jizatiti katika mji wa Bani Walid na Bonde nyekundu, ambayo ni eneo muhimu sana kwa ngome ya Sirte.

Mapigano makali yaliripotiwa baina ya pande hizo mbili na kumalizika alasiri, huku kila upande ukishindwa kumrudisha mwenzie nyuma.

Katika kutoa muda wa siku 10 kw awafuasi wa Gaddafi kujisalimisha baraza la mpito nchini Libya lilikuwa na dhamira ya kuepusha umwagaji damu. Kwa muda wa siku kumi wa majadiliano bila hata hivyo kufikia muafaka.

Kwenye uwanja wa mapambano jazba ilianza kupanda hata kabla ya muda kumalizika. Matumizi ya kijeshi sasa yaonekana kutiwa mbele. Mahmoud Jibril Naibu kiongozi wa baraza kuu la waasi alikuwa muwazi sana pindi aliposema kwamba ” Mapambano hayajafikia kikomo. Tunayo haki ya kujihami na kuokowa taifa nzima la Libya”

wanajeshi wote wa utawala mpya wamewekwa katika hali ya taharuki kuanzisha mapambano ya kumalizia kabisa ngome ya mwisho ya wanajeshi tiifu kwa kanali Muamar Gaddafi.

Swala lilipo ni kujuwa idadi ya wanajeshi wa kanali Gaddafi na wapi waupata uwezo. Katika kushambulia Septemba 8 katika ngome zote mbili , wafuasi wa Gaddafiwaonyesha ukakamavu wao. Ishara ya kwamba wakotayari kupigana hadi mwisho

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.