Pata taarifa kuu
Zimbabwe

Rais Mugabe asema waangalizi kutoka Uingereza na Umoja wa Ulaya hawatokuwa na nafasi nchini mwake

Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe, amesema serikali yake haitaruhusu waangalizi kutoka Uingereza na Umoja wa Ulaya kushuhudia uchaguzi  mkuu nchini humo ambao hadi sasa haujafahamika utafanywa lini.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mugabe amesema, uamuazi huo umechukuliwa kwa sababu serikali yake haitaki waangalizi ambao anasema huenda wataegemea upande mmoja wakati wa uchaguzi huo.

Serikali ya muungano ya Zimbabwe imekuwa ikikabiliwa na changamoto za uongozi kati ya rais Mugabe na Waziiri Mkuu Morgan Tshangirai, tangu mwaka wa 2008, na rais Mugabe amenukuliwa mara kwa mara akisema kuwa, uchaguXi mpya ndio unaoweza kutatua tatizo hilo.

Lakini Tshangirai anatofautiana naye kwa kile anachokisema kuwa uchaguzi huru na haki unaweza kufanyika tu ikiwa taifa hilo litapata katiba mpya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.