Pata taarifa kuu
Ujerumani-Marekani

Watu 2 wakamatwa mjini Berlin kwa tuhuma za kumiliki kemikale zinazoweza kutengeneza bomu

Mamkala nchini Ujerumani katika Jiji la Berlin limewakamata watuhumiwa wawili wakiwa na kemikali ambazo zinaelezwa huenda zikatumika kama bomu wakati huu ambapo maadhimisho ya muongo mmoja wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Marekani yakiendelea.

Polisi mlangoni mwa msikiti mmoja katika eneo la Wedding nchini Ujerumani
Polisi mlangoni mwa msikiti mmoja katika eneo la Wedding nchini Ujerumani LE VIF EXPRESS
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Polisi limemkamata raia wa Ujreumani mwenye asili ya Lebanon mwenye umri wa miaka ishirini na nne pamoja na Mpalestina mwenye umri wa miaka ishirini na nane kwa tuhuma za kutengeneza mlipuko huo wa bomu.

Taarifa kutoka Mamlaka nchini Berlin zinaweka bayana kuwa watu hao wamenaswa kutokana na kuimarishwa kwa usalama katika nchi hiyo wakati huu ambapo kumekuwa na hofu huenda kukafanyika mashambulizi kutoka kwa makundi ya kigaidi.

Watuhumiwa hao walikuwa wafuasi wa msikiti mmoja katika katika mji wa Wedding ambako mara kadhaa walikuwa waki lala ndani ya muskiti huo
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.