Pata taarifa kuu
SYRIA-POLAND

Vikosi vya Serikali ya Syria vya waua waandamanaji 20

Vikosi vya serikali ya Syria vimewaua waandamanaji wanaokadiriwa kufikia ishirini katika maandamano yanayoendelea kusambaa kwenye nchi hiyo wakati huu ambapo Umoja wa Ulaya EU umeweka vikwazo vya kununua mafuta yasiyosafishwa kutoka katika nchi hiyo.

Reuters/Handout
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati ambao wameandaa maandamano hayo yanayochagizwa na kaulimbiu ya “Bora Kifo Kuliko Ukandamizaji” wamesima wamekutana na upinzani mkali kutoka kwa majeshi ya serikali ya Rais Bashar Al Assad.

Wanaharakati nchini Syria wamekiri kuridhishwa na mwitikio wa wananchi ambao wamejitokeza kwenye maandamano hayo yenye lengo la kushinikiza mabadiliko ya utawala nchini mwao.

Taarifa za vifo hivyo zimetolewa na Wanaharakati zikonesha kuwa watu wanane wameuawa na majeshi ya serikali katika maeneo ya Douma na Erbeen wakati wakiwa kwenye maandamani ya amani.

Televisheni ya Taifa ya Syria SANA imeonesha watu wawili tu ndiyo wameuawa kwenye operesheni ya kijeshi ya kuzima maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea kwenye miji mbalimbali kwa sasa.

Licha ya majeshi ya serikali kuendelea na kampeni ya kuwafunga mdomo waandamanaji lakini taarifa zinasema kuwa wanajeshi watatu wameuawa na Makundi ya Kigaidi yanayofanya mashambulizi katika maeneo ya Talbisseh, Erbeen na Hammuriyeh.

Haya yote yanashika kasi wakati ambapo Umoja wa Ulaya EU umeongeza vikwazo dhidi ya Rais Assad pamoja na wale wanaomuunga mkono wakiwemo wafanyabiashara ambao nao wamezuiliwa kusafiri na hata mali zao kuzuiliwa.

Ufaransa nayo inatarajiwa kuongeza vikwazo hivyo kwani inatarajiwa kutangaza kumtenga Rais Assad na kuongeza juhudi katika kuwasaidi wapinzani nchini Syria ambao wanataka demokrasia ya kweli.

Nao Mawaziri kutoka nchi wanachama 27 za Umoja wa Ulaya EU wanatarajiwa kutoa kauli yao juu ya kile ambacho kinaendelea nchini Syria pindi watakapomaliza kikao chao kinachofanyika huko Poland.

Tangu kuanza kwa maandamano ya wanaharakati nchini Syria takwimu za Umoja wa mataifa UN zinaonesh watu zaidi ya 2200 wameshauwa katika miji ya nchi hiyo huku kubwa likiwa ni kushinikizwa kwa mabadiliko ya uongozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.