Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-ISRAELI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN azitaka Uturuki na Israeli kurejesha uhusiano wao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amezitaka nchi za Uturuki na Israel kurejesha uhusiano wao ikiwa ni siku moja baada ya Ankara kumtimua Balozi wa Israel katika nchi hiyo.

REUTERS/Truth Leem
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu Ban amesema mataifa hayo mawili yanastahili kurejesha uhusiano wake wa kidiplomasia kwa kuwa ni wadau muhimu sana katika upatikanaji wa usalama na amani ya kweli katika eneo la mashariki ya kati.

Ban amewaambia wanahabari ana matumaini pande hizo mbili yaani Israel na Uturuki zitakaa pamoja na kumaliza tofauti zao zilizojitokeza baada ya kushambuliwa kwa meli ya Uturuki iliyokuwa inapeleka misaada Ukanda wa Gaza.

Katibu Mkuu wa UN ameweka bayana nchi hizo mbili yaani Israel na Uturuki ni muhimu sana katika kufanikisha mpango wa upatikanaji wa amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Ban amesema yupo tayari kuingilia kati mgogoro huo na kushiriki ipasavyo katika kurejesha uhusiano ambao umeingia dosari tangu kutokea kwa shambulizi la meli ya misaada ya Uturiki mapema mwezi may mwaka 2010.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN amesema hawezi kutoa maoni yoyote juu ya kile kinachoendelea baina ya nchi hizo za Israel na Uturuki kwa sasa lakini kubwa ambayo anataka kuliona ni kurejea kwa uhusiano huo.

Mgogoro baina ya Israel na Uturuki umeibuka upya baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa UN kuweka bayana makomandoo wa Israel walitumia nguvu kubwa kuizuia meli ya Uturuki ambayo ilikuwa inapeleka misaada katika eneo la Ukanda wa Gaza.

Makomandoo wa Israel waliishambulia meli ya misaada ya Uturuki mnamo tarehe 31 ya mwezi May mwaka 2010 na kusababisha vifo vya wanaharakati tisa waliokuwemo kwenye meli hiyo.

Lakini hatua ya kutimuliwa kwa Balozi wa Israel nchini Uturuki imekuja baada ya nchi hiyo kukataa kuomba kwa kutokana na kutekeleza shambulizi hilo na kusababisha vifo kwa wanaharakati hao tisa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.