Pata taarifa kuu
SYRIA

Wanaharakati nchini Syria waitisha maandamano makubwa wakati Marekani wakisisitiza Rais Assad aondoke madarakani

Vikosi vya serikali nchini Syria vimeendelea kufanya mauaji zaidi na taarifa zinaweka bayana watu saba wamepoteza maisha wakati huu ambapo wanaharakati nchini humo wameitisha maandamano yenye kaulimbiu “Bora kifo kuliko Ukandamizaji”.

(REUTERS)
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati nchini Syria wamethibitisha kutokea kwa vifo hivyo vya watu saba wakati huu ambapo wananchi wanaopinga Utawala wa Rais Bashar Al Assad wakiongeza shinikizo la kusikilizwa kwa kili chao.

Makundi ya Wanaharakati yameitisha maandamano makubwa hii leo katika Miji mbalimbali nchini Syria baada ya sarat Ijumaa kutaka Jumuiya ya Kimataifa kuweza kuchukua hatua dhidi ya mauaji ambayo yanafanyika kwenye taifa hilo.

Uamuzi wa kuitisha maandamano hayo unakuja wakati hapo jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akiendelea na msimamo wa nchi yake wa kutaka mapigano yasitishwe na Rais Assda akae kando.

Waziri Clinton amesema ni jukumu la Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha wanachukua hatua kuweka vikwazo kwenye biashara ya mafuta na gesi ya Syria inayosafirishwa kwenye mataifa mbalimbali.

Naye Waziri Mkuu wa Uhispania Jose Luis Rodriguez Zapatero ametoa kauli ya kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwaunga mkono wapinzani nchini Syria na hata kuchukua hatua zilizochukuliwa na Umoja wa mataifa UN dhidi ya Libya.

Kauli za viongozi hawa vinakuja wakati ambapo Mawaziri wa Mambo ya Nje wakitarajiwa kukutana kujadili hatua ya kuiwekea vikwazo zaidi nchi ya Syria ambayo kila kukicha imeendelea kushuhudia mauaji ya kutisha.

Takwimu za Umoja wa Mataifa UN zinaonesha zaidi ya watu elfu mbili na mia mbili wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mafuko nchini Syria ya kutaka mabadiliko ya utawala na utekelezaji wa demokrasia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.