Pata taarifa kuu
SYRIA

Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Hama nchini Syria ajiuzulu wadhifa wake kutokana na ghasia zinazoendelea

Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Hama nchini Syria Mohammed Adnan Al-Bakkour ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kuendelea kwa machafuko na kuchangia vifo vya mamia ya wananchi na wengine wakikamatwa kutokana na kufanya maandamano.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Al-Bakkour amethibitisha kujiuzulu wadhifa wake katika taarifa ambayo imetolewa katika vyombo vya habari akisema amejitoa katika Utawala wa serikali inayoongzowa na Rais Bashar Al Assad.

Mwanasheria huyo wa zamani wa Jimbo la Hama amesema uamuzi wake ameutoa baada ya kuona mamia ya wafungwa waliokamatwa kwenye maandamano nchi humo kuuawa na Mamlaka na kisha kuzikwa kwenye kaburi la pamoja.

Kwa mujibu ya video ambayo imesambazwa inaonesha namna ambavyo Al-Bakkour alivyotangaza hatua yake ya kujiuzulu wadhifa wake lakini serikali imepinga vikali kama huo ni uamuzi wake.

Serikali ya Syria kupitia Chombo chake cha Habari cha SANA kimesema uamuzi huo wa Al-Bakkour umekuja baada ya kutekwa akiwa njiani kueleka kazini kwake na hivyo kulazimishwa kutoa kauli hiyo.

Taarifa hizo kutoka serikali ya Rais Al Assad zimeweka bayana kauli hiyo imetoka wakati Al-Bakkour akiwa amewekewa silaha na hivyo kulazimika kutangaza kujiuzulu wadhifa wake kwa kushurutishwa.

Serikali imeendelea kutoa taarifa ya kwamba Mwanasheria Mkuu huyo wa Jimbo la Hama amelazimishwa pia kusema zaidi ya watu mia nne na ishirini walizikwa kwenye kaburi la pamoja baada ya kuuawa na Mamlaka nchini humo.

Kauli ya serikali imezua mgongano nchini Syria ambapo wengine wanaamini serikali inataka kukanusha ili iendelee kujitakasa mbele ya macho ya Jumuiya ya Kimataifa lakini ukweli hali ni mbaya nchini humo.

Kwa upande mwingine Wanaharakati nchini Syria wamesema watu zaidi ya mia nne na sabini wameuawa siku ya jumatano wakati vifaru vya kijeshi vya serikali vilivyofanya mashambulizi kuwadhibiti waandamanaji.

Takwimu za Umoja wa Mataifa UN zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu mbili na mia mbili wamepoteza maisha nchini Syria tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga Utawala wa Rais Al Assad.

Mataifa ya Magharibi hadi sasa yameishia kutangaza vikwazo tu dhidi ya Rais Al Assad na kumtaka ajiuzulu kwa kuwa amepoteza uhalali wa kutawala nchi hiyo lakini mwenyewe ametia ngumu kutekeza shinikizo hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.