Pata taarifa kuu
Sudani ya Kusini-Mapigano

Mapigano ya kugombea ng'ombe yauwa watu zaidi ya 130 Sudani ya Kusini

zaidi ya watu mia themanini na watano wameuawa Sudan kusini katika mapambano ya kugombea ng'ombe, halikadhalika shambulio la watu wenye silaha,maafisa wa nchini humo wamethibitisha.

Nenda rudi ya watu wenye silaha
Nenda rudi ya watu wenye silaha france24
Matangazo ya kibiashara

Matukio hayo yanadhihirisha namna sudani kusini ilivyo na changamoto ya usalama ulio tete baada ya taifa hilo kujitwalia uhuru wake mwezi julai.

msemaji wa jeshi la sudani kusini, kanali Philip Aguer amesema wapiganaji wanaomtii kiongozi wa waasi George Athor wameshambulia jimbo la Nile lililopo nchini humo na kuongeza kuwa mapigano hayo yalianza siku ya ijumaa na kugharimu maisha ya watu 60.

katika tukio jingine maafisa wa nchi hiyo wamethibitisha kuwa watu mia moja ishirini na watano waliuawa katika mapambano ya kugombea Ng'ombe kati ya makabila mawili hasimu ya Murle na luo- nuer ambapo takriban ng'ombe 2000 waliibwa mashariki mwa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.