Pata taarifa kuu
SYRIA

Majeshi ya Syria yaanza kuondoka katika baadhi ya miji iliyokuwa inaishikilia

Maandamano zaidi yameendelea nchini Syria usiku wa kuamkia leo licha ya operesheni za kijeshi zinazoendelea kufanywa na vikosi vya nchi hiyo katika miji kadhaa yneye vurugu ukiwemo mji wa Latakia ambao kwa siku tatu mfululizo ulikuwa katika hali ya sintofahamu.

Smoke rises in the city of Latakia August 14, 2011.
Smoke rises in the city of Latakia August 14, 2011. Reuters路透社
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya usiku wa kuamkia leo yameshuhudiwa katika miji ya Homs, Albu Kamal mpakani na nchi ya Iraq pamoja na baadhi ya vitongoji vya mji mkuu Damascus ambako vifo vimeripotiwa kutokana na maandamano hayo.

Siku ya jumanne waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Brigedia Jenerali Mohammad Hassan al-Ali alitangaza majeshi ya nchi yake kumaliza operesheni katika maeneo ya al-Ramel mji ulioko jirani na mji wa Latakia ambao umekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa siku tatu mfululizo.

Waziri huyo ameongeza kuwa hivi sasa maisha ya wananchi katika maeneo hayo yameanza kurejea katika hali ya kawaida baada ya kusitishwa kwa operesheni za kijeshi na kuwataka wananchi kurejea katika makazi yao.

Wanaharakati nchini humo wameendelea kuonyesha hofu yao kuhusu operesheni za kijeshi zinazofanywa katika mji wa Latakia na kudai kuwa endapo wananchi hao wakirejea watakamatwa na polisi ambao bado wameonekana katika sehemu za mji huo.

Hata hivyo maandamano ya usiku wa kuamkia leo yamefanywa kwa lengo la kuendelea kuishinikiza serikali ya rais Bashar al-Assad kuondoka madarakani na kupisha serikali ya mpito wito ambao rais Assad mwenyewe amekataa katakata kutekeleza matakwa ya waandamanaji.

Wakati serikali ikitangaza kumaliza operesheni katika mji wa Latakia bado kumesikika milio ya risasi katika baadhi ya sehemu ya mji huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.