Pata taarifa kuu
LATAKIA-SYRIA

Hali ya sintofahamu yaendelea kutawala mjini Latakia, Syria

Wakati jumuiya ya kimataifa ikiendelea kutoa wito kwa serikali ya Syria kuacha kutumia nguvu dhidi ya raia wanaofanya maandamano ya amani, bado wanajeshi wa nchi hiyo wameendelea na operesheni katika mji wa Latakia na kusababisha maelfu kuanza kuukimbia mji huo.

Vifaru vya majeshi ya Syria katika mji wa Hama
Vifaru vya majeshi ya Syria katika mji wa Hama Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo ya vikosi vya serikali ambayo yamedumu kwa siku ya tatu mfululizo yameshuhudia maelfu ya wananchi wakiyakimbia makazi yao kuelekea mpakani mwa nchi hiyo na Lebanon wakihofia mashambulizi zaidi pamoja na kukamatwa.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini Syria yamesea kuwa vikosi vya nchi hiyo vimeendelea kuwakamata maelfu ya wananchi ambao wanakimbia mji huo na kuwaweka kizuizini huku baadhi yao wakiripotiwa kupigwa risasi pale wanaposhindwa kutii amri ya kusimama.

Watetezi hao wa haki za binadamu wamesema kuwa mabasi ya jeshi la nchi hiyo ndio yamekuwa yakitumika kuwapeleka wananchi hao katika uwanja mmoja maalumu amabo umetengwa na vikosi hivyo kwa wananchi hao kuhifadhiwa kabla ya kupelekwa mjini Damascus kusomewa mashtaka ya kufanya maandamano.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa nchini humo Chris Gunness amesemas kuwa maofisa wake wameshuhudia zaidi ya wananchi 5000 hado 10000 raia wa Palestina waliokuwa wanaishi nchini humo wakiukimbia mji wa Latakia na kuingia katika mji wa al-Ra,el amabko kumefunguliwa kambi ya muda kwaajili ya kuwahifadhi wakimbizi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.