Pata taarifa kuu
Libya

Serikali ya Gaddafi yaishutumu NATO kutekeleza mauaji ya mama na wanae 2

Wakati maofisa wa serikali ya Libya, wakidai kuwa majeshi ya Umoja wa Kujihami wa nchi za magharibi NATO, yameua mwanamke mmoja na watoto wake wadogo wawili, vikosi vya Kanali Muamer Gaddafi vinaushikilia mji wa Zlitan.

Moja ya ndege za kivita za NATO
Moja ya ndege za kivita za NATO Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia tuhuma hizo na majeshi ya NATO, yanachunguza ili kuujua ukweli.

Mafaanikio hayo yamekuja baada ya majeshi ya kiongozi huyo, anayekaidi wito wa kuondoka madarakani, kulipiza mapigo ya waasi, wanaopambana na serikali, wakisaidiwa na majeshi ya NATO, tangu mwezi Machi, mwaka huu.

Kwa majuma kadhaa yaliyopita, waasi wamekuwa wakikaribia jiji hilo, taratibu, kutokea Misrata, kilomita 70 hivi mashariki mwa Libya.

Baada ya Zlitan, nia yao ni kusogea mbele zaidi takriban kilomita 160 hivi, pembeni mwa barabara inayoelekea Tripoli.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.