Pata taarifa kuu
Umoja wa Ulaya

EU yataka utekelezwaji wa makubaliano ya kuunda sera ya pamoja kw amataifa ya G7 NA G20

Umoja wa Ulaya, umeyataka mataifa tajiri uliwenguni ya G7 na G20 kutekeleza mara moja mapendekezo waliyoafikiana mwezi uliopita ya kuunda sera ya pamoja ya kukabiliana na madeni ya jumuiya hiyo ,ili kutatua ongezeko la madeni katika mataifa hayo yanayotishia hatari ya kuporomoka kwa uchumi wa mataifa ya ulaya.

Kamisheni wa EU anaehusika na maswala ya kiuchumi Olli Rehn
Kamisheni wa EU anaehusika na maswala ya kiuchumi Olli Rehn Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kamishna wa jumuiya hiyo, anayehusika na maswala ya kiuchumi Olli Rehn amesema mtikisiko wa uchumi unaoshuhudiwa barani Ulaya unaonekana kuathiri mataifa mengine duniani kutokana na kushuka kwa masoko ya hisa. Olli amesema, mpango huo wa kunusuru uchumi wa ulaya unastahili kufikiwa mwezi Septemba.

Wachambuzi wa maswala ya kiuchumi nao wanahisi kuwa, muafaka unachukua muda kufikiwa kwa sababu kila mmoja anavutia upande wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.