Pata taarifa kuu
MAREKANI

Rais Obama awatupia lawama wabunge wa Republican

Rais wa Marekani Barack Obama ameendelea kuwalaumu wabunge wa chama cha Republican kwa kusababisha mpaka sasa nchi hiyo kushindwa kufukia muafaka kuhusu kupitishwa kwa bajeti ya kubana matumizi ili kuinusuru nchi hiyo na mgogoro wa kifedha.

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama REUTERS/Jim Watson/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama amekuwa katika mazungumzo na wabunge wa republican tangu juma lililopita mabpo ni juma lililoisha imeshuhudiwa mazungumzo kati yake na wabunge hao yakivunjika kutokana na kutoelewana.

Akiongelea kauli ya rais Obama, spika wa bunge la republican John Boehner amesema kuwa wabunge wa chama chake watapiga kura kupitisha mapendekezo ya serikali endapo serikali ya rais Obama itakubalina na mapendekezo ambayo waliyatoa ya kuongeza bei katika baadhi ya huduma muhimu.

Hapo jana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton aliwataka wabunge wenzake kupunguza jazba na kuwa kitu kimoja katika kuinusuru nchi hiyo kuingia katika mgogoro wa kifedha na kuifanya nchi hiyo kujiweka katika wakati mgumu kukuza uchumi wake.

Wabunge hao wanasiku chache hadi kufikia tarehe 2 mwezi wa 8 mwaka huu kuhakikisha wanapitisha mapendekezo ya serikali ya kubana matumizi kwa zaidi ya dola bilioni 14 ili kuinusuru nchi hiyo kutumbikia katika mgogoro wa kifedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.