Pata taarifa kuu
Libya - marekani

Serikali ya libya yasema ipo tayari kuzungumza na waasi lakini haitaki masharti yoyote

Licha ya juhudi za mataifa ya ulaya kushinikiza viongozi wa serikali ya Libya kufanya mazungumzo na waasi kwa lengo la kutafuta suluhu nchini humo, viongozi wa nchi hiyo wameendelea kukataa masharti yoyote yanayotolewa na waasi ili kutekeleza mazungumzo hayo.

Waasi wa libya wakiwa njiani kuelekea mji wa bandari wa Brega Julay 18, 2011.
Waasi wa libya wakiwa njiani kuelekea mji wa bandari wa Brega Julay 18, 2011. AFP/Gianluigi Guercia
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya serikali ya Libya imekuja ikiwa zimepita saa chache baada ya maofisa wa serikali ya Marekani kukutana na viongozi wa serikali ya kanali Muamar Gaddafi na kusisitiza  kiongozi huyo kung'atuka madarakani.

Ujumbe huo wa Marekani umesema kuwa lengo ls kukutana na viongozi wa serikali ilikuwa ni kusisitiza msimamo wa nchi yao ambao unataka kuona kanali Gaddafi anaondoka madarakani kabla ya kufanyiks mazungumzo yoyote ya kutafuta suluhu.

Mazungumzo hayo yamefanyika wakati ambapo Ijumaa iliopita Marekani ilitangaza kuwatambua waasi wa Libya kama mamlaka rasmi ya nchi hiyo na kuahidi kuendelea kuwasaidia hadi wanafikia malengo yao.

Wakati huohuo mapigano yamepamba moto baina ya vikosi vya serikali ya vile vya waasi katika mji wa bandari na utajiri wa mafuta wa Brega. Hapo jana waasi walitangaza kuuteka mji huo na baadae serikali ya Libya kukanusha. Hadi sasa ni vigumu kujuwa nani anatawala mji huo kati ya serikali ya Kanali Muamar Gaddafi na waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.