Pata taarifa kuu
Afghanistani

Rais wa Afghanistani aongoza shughuli za mazishi ya nduguye mjini Kaboul

Maelfu ya wananchi wakiongozwa na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai leo wamejitokeza katika mazishi ya Ahmed Wali Karzai mdogo wa rais wa nchi hiyo aliyeuawa siku ya jumanne mjini Kandahar.

Hamid Karzai akiongoza shughuli za mazishi ya ndugu yake
Hamid Karzai akiongoza shughuli za mazishi ya ndugu yake Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Karzai aliwaongoza maelfu ya wananchi hao katika mazishi ya mdogo wake huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika eneo hilo kwa ndege za majeshi ya NATO kwa kushirikiana na vikosi vya serikali wakionekana kupiga doria kwa muda wote wa wa mazishi.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa mapema kabla ya kufanyika kwa mazishi hayo kulisikika milio ya risasi na mabomu ambapo gavana wa jimbo la helmand Gulab Mangal alinusurika kifo katika shambulio lililolenga gari alilokuwa akitumia .
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.