Pata taarifa kuu
Marekani - Urusi

Marekani yaunga mkono juhudi za Urusi za kuutanzua mzozo wa Libya

Marekani itaunga mkono mpango wa urusi kuutatua mzozo wa Libya mpaka kiongozi wa nchi hiyo Muamar Gaddafi atakapoachia madaraka.

Barack Obama rais wa Marekani Julay 10, 2011.
Barack Obama rais wa Marekani Julay 10, 2011. REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Rais wa marekani Barak Obama amemshukuru Rais wa Urusi Dimitry medvedev hapo jana kwa juhudi za upatanishi nchini Libya na kusisitiza kuwa Marekani inajiandaa kuunga mkono hatua hiyo itakayofungua njia ya mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Gaddafi kuachia madaraka.

Obama aliongea na medvedev juu ya maswala yahusuyo nchi hizo mbili, maswala ya kimataifa na kutoa salamu za rambirambi baada ya ajali ya boti iliyotokea katika mto volga nchini Urusi.

Urusi ilipinga mpango wa kupigia kura azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililofungua milango kwa mataifa ya magharibi kujihusisha na mgogoro wa Libya na imekuwa ikikosoa kampeni ya majeshi ya NATO nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.