Pata taarifa kuu
Syria

Serikali ya Bashar Al Assad yaishutumu Marekani kuchochea ghasia nchini Syria

Licha ya shinikizo toka jumuiya ya kimataifa kuvitaka vikosi vya serikali ya Syria kusitisha vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu, serikali ya Rais Bashar al-Assad imeendelea kuishutumu nchi ya Marekani kwa kuchochea vurugu nchini humo.

Waziri wa Syria wa mambo ya kigeni
Waziri wa Syria wa mambo ya kigeni REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria ikilaumu ziara ambayo ilifanywa na balozi wa marekani nchini humo katika mji wa Hama.

Taarifa hiyo imeitaka nchi ya Marekani kutoingilia maswala yake ya ndani na kutishia kuvunja uhusiano wa kibalozi endapo itaendelea kuingilia mambo ya nchi hiyo.

Maelfu ya wananchi wameanza kuukimbia mji huo kufuatia kuitishwa kwa maandamano makubwa hii leo mara baada ya kumalizika kwa sala ya mchana, maandamano yanayolenga kupinga mazungumzo yoyote yaliyoitishwa na serikali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.