Pata taarifa kuu
Afghanistani

watu 13 wapoteza maisha huko Afghanistani

Takriban raia kumi na watatu wa Afghanistan wengi wao wanawake na watoto wameuawa kwa shambulio lililofanywa hii leo na jumuia ya majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi, NATO huko khost nchini afghanistan.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa polisi mjini Khost,Mohamad Zazai amesema mpaka sasa wanawake wanane, watoto wanne na mwanaume mmoja,wameuawa na majeshi hayo kwa shambulio la anga lililopiga nyumba moja asubuhi ya leo.

Taarifa zinasema kuwa wanamgambo wanne wa kundi la taliban nao wameuawa katika shambulio hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.