Pata taarifa kuu
Italia - Libya

Italia kuondowa ndege zake za kivita katika operesheni ya NATO nchini Libya

Serikali ya Italia inaondoa ndege zake za kijeshi kutoka nchini Libya zilikokuwa zikishiriki operesheni ya NATO, kupambana na vikosi vya kiongozi wa taifa hilo, Muamar Gaddafi.

LADEPECHE.fr
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa Italia, Ignazio la Russa amesema Hatua hiyo imekuja zikiwa ni juhudi za kubana matumizi ya gharama za kiasi cha euro milioni 80.na kutangaza kuwa pia wanampango wa kuondoa meli yao kutoka kwenye mpango wa operesheni hiyo.

Taarifa hizo zimekuja baada ya baraza la mawaziri la Italia kukubaliana kupunguza matumizi ya kijeshi kwa kuondoa ndege zake za kijeshi nchni Libya kwa kile walichodai kuwa hazina ulazima wa kuwepo nchini humo tena.

Kutokana na mtikisiko wa kiuchumi ulioukumba italia,serikali ya nchi hiyo imelazimika kubana matumizi hasa kupunguza operesheni zake za kijeshi nje ya nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.