Pata taarifa kuu
CHINA

Mwanaharakati Hu Jia aachiliwa huru

Serikali ya china imemuachilia huru mwanaharakati Hu Jia ambaye ametumikia kifungo cha mika mitatu na nusu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya serikali.

Mwanaharakati Hu Jia akiwa na mkewe
Mwanaharakati Hu Jia akiwa na mkewe Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Hu mwenye umri wa miaka 37 hivi sasa alikuwa mmoja wa wanaharakati wa mazingira na mtu aliyekuwa mstari wa mbele kupigania haki za raia harakati zilizopeleka kujikuta gerezani baada ya mahakama kumkuta na hatia.

Mwanaharakati huyo alikamatwa mjini Beijing baada ya kuikosoa serikali na kudai kuwa ni moja kati ya serikali zinazokiuka haki za binadamu kwa kutowajali wananchi wake na kuwanyima uhuru wa kufanya mikutano.

Hu ambaye kifungo chake kilikuwa kimalizike siku ya jumapili aliachiliwa jana jioni na kuungana na familia yake huku wachambuzi wa mambo wakisema kuwa huenda kumechangiwa na ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao nchini uingereza ambapo swala la haki za binadamu linatarajiwa kuchukua nafasi katika mazungumzo yake na waziri mkuu Cameron.

Nchi ya China imekuwa mara kadhaa ikikosolewa na jumuiya ya kimataifa kwakutoheshimu haki za binadamu huku ikiongoza kwa kunyonga watu wanaopatikana na hatia ya kufanya maandamano yasiyoruhusiwa ama vitendo vya rishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.