Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Watu zaidi ya 30 wamekufa katika shambulio la kujitoa muhanga nchini Afghanistan

Watu zaidi ya 30 wamekufa na wengine zaidi ya 120 wamejeruhiwa vibaya kufuatia shambulio la bomu la kujitoa muhanga lililotekelezwa katika hospitali moja kusini mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul wizara ya afya imedhibitisha.

Askari wa Afghanistan wakiwa katika doria mjini Kabul baada ya shambulio la bomu
Askari wa Afghanistan wakiwa katika doria mjini Kabul baada ya shambulio la bomu Reuters/Ahmad Masood
Matangazo ya kibiashara

Maofisa usalama nchini humo wamesema kuwa shambulio hilo limetekelezwa na mtu ambaye alitumia gari dogo kufanya tukio hilo ambapo alisogea hadi eneo la hospitali na kujilipua na kuua watu 30 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Taarifa hiyo imetolewa muda mchache uliopita na wizara ya afya ikirekebisha idadi ya awali ya watu walioshukiwa kufa kutoka 60 hadi 30 kulingana na taarifa za maofisa wa usalama zilizopelekwa kwa waziri wa mambo ya ndani.

Tukio hilo la kujitoa muhanga limekuja ikiwa zimepita siku chache tangu rais wa Marekani Barack Obama atangaze mpango wa kuviondoa vikosi vyake vya wanajeshi zaidi ya elfu kumi nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, huku vikosi zaidi vikitarajiwa kuondoka nchini humo kabla ya 2014.

Kufuatia shambulio hilo katika mji wa Logar, msemaji wa mji huo Din Mohammad Dar amesema kuwa tayari serikali ya nchi hiyo imeomba msaada toka vikosi vya kigeni vilivyoko nchini humo kuwasaka waliohusika na shambulio hilo ikiwemo kutoa wataalamu wa afya kuwatibu waliojeruhiwa.

Maofisa wa polisi katika mji huo wamesema kuwa hili ni shambulio kubwa zaidi kwa mwaka huu kutekelezwa ambapo wamelitaja kundi la Taliban kuhusika katika shambulio hilo la hii leo.

Hata hivyo wakati viongozi wa mji wa Logar wakilitaja kundi la taliban kuhusika katika shambulio hilo, msemaji wa kundi hilo, Zabihullah Mujahid amekana kundi lake kuhusika katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni imesema kuwa watu zaidi ya laki mbili waliuawa kwa mwaka jana peke yake

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.