Pata taarifa kuu
Libya-Tripoli

Kiongozi wa Libya Mouamar Gaddafi avishutumu vikosi vya NATO kwa kuendesha mauaji ya raia nchini mwake

Kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi ameyalaumu majeshi ya kujihami ya umoja wa nchi za magharibi, NATO kwa mauaji ya raia yanayotekelezwa nchini mwake na majeshi ya NATO.  

Kiongozi wa libya Muamar Gaddafi
Kiongozi wa libya Muamar Gaddafi ©Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Gaddafi imekuja baada ya NATO kufanya mashambulizi mfululizo na kuua raia wakiwemo watu wa familia ya msaidizi wake wa karibu na amesema vitendo hivyo ni kinyume na haki za binadamu.

Gaddafi amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na NATO havitawazuia wao kupambana mpaka dakika ya mwisho na wako tayari kufa katika kukabiliana na vitendo hivyo.

Kiongozi huyo wa Libya amesema kuwa mashambulizi ya NATO ni haramu na wanaoshiriki kuua watu wa Libya ni wahalifu wanaolenga kuiangamiza Libya na watu wake.

Majeshi ya NATO yamekiri kuhusika na baadhi ya vifo vya raia lakini hayawalengi raia moja kwa moja kama inavyodaiwa na serikali ya Muammar Gadaffi.

Katika hatua nyingine, Serikali ya Italia imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia watu walioathirika na vita.

Wito huo umetupiliwa mbali naUongozi wa majeshi ya NATO unasema hautasitsiha mashmabulizi yake dhidi ya majeshi ya Muamar Kadhafi nchini Libya,licha ya ombi kutoka kwa Italia inayotaka mashambulizi hayo kusimamihswa kwa muda ili msaada wa kibiandamu uwafikie waathiriwa wa mashambulizi hayo.

Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen,amesema mashambulizi hayatakoma kwa kile anachokisema kuwa yakisitishwa,huenda mauji zaidi ya raia yakashhudiwa huko Libya.

Wito sawa na huo umetolewa na Amr Moussa mwenyekiti wa nchi za kiarabu. Ufaransa nayo inasema mashambulizi hayo hayastahili kusistishwa,lakini wachambuzi wa mambo wnasema kuwa ikiwa lengo la NATO lilikuwa ni kulinda raia basi hawana budi kusitisha mashambulizi hayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.