Pata taarifa kuu
JAPAN

Wataalamu Japan waendelea kupoza vinu vya Fukushima

Ni miezi mitatu sasa imepita tangu kushuhudia nchi ya Japan ikikumbwa na tetemeko kubwa la Ardhi lililosababisha maafa nchini humo ikiwemo watu kufa na kupasuka kwa vinu vya Nyuklia vya Fukushima.

Eneo ilipo mitambo ya Nyuklia ya Fukushima Daiichi
Eneo ilipo mitambo ya Nyuklia ya Fukushima Daiichi Reuters/Air Photo Service/Files
Matangazo ya kibiashara

Ni tukio ambalo kamwe ulimwengu hauwezi kulisahau kirahisi kutokana na athari zake kuwa kubwa kwa wananchi wa taifa hilo na dunia kwa ujumla huku ikielezwa kuwa zaidi ya watu elfu kumi na tano walipoteza maisha katika Tsunami hiyo.

Hivi sasa wataalamu wa masuala ya Nyuklia nchini Japan wanaendelea na juhudi za kupoza mitambo ya Fukushima ambayo mara baada ya tetemeko la Ardhi ililipuka.

Wataalamu hao wameongeza kuwa wanatarajia ifikapo katikati ya mwezi wa Sita watakuwa wamefanikisha kwa kiwango kikubwa kudhibiti uvujaji na kupooza mitambo hiyo.

Tangu kufanikiwa kwa wataalamu hao kudhibiti kuvuja kwa mionzi ya Nyuklia, wamekuwa katika hatua mablimbali za kitaalamu kuendelea kupoza vinu ambayo bado havijapoa na vilikuwa katika hatari ya kulipuka na kuongeza kuwa mpaka kufikia tarehe hiyo watakuwa wamefunga mitambo maalumu ya kupoza vinu vyote.

Kwasasa wataalamu hao wamesema kuwa wanaendelea kufunga baadhi ya mashine za kupoza vinu hivyo na kuendelea kuvuta maji kuyapeleka katika mitambo hiyo kwa lengo la kupunguza mionzi zaidi.

Shirika la umeme nchini humo la TEPCO ambalo linazalisha umeme kwa kutumia mitambo hiyo, limetoa taarifa inayoonyesha kuwa mpaka kufikia katikati ya mwezi wa sita watakuwa wamefanikiwa kudhibiti mitambo yote na hali kurejea kama awali.

Kutokea kwa tukio hilo kumeyumbisha serikali ya waziri mkuu Naoto Kan ambaye juma lililopita alishinda kura ya kutokuwa na imani nae.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.