Pata taarifa kuu
Libya, Tripoli

NATO yapewa muda zaidi kuhudumu nchini Libya

Vikosi vya kujihami vya nchi za magharibi NATO vimekubali pendekezo la kuongeza muda wa vita ya angani nchini Libya kwa kipindi cha miezi mitatu huku kikitupilia mbali shutuma zilizo tolewa na serikali ya Gadaffi kwamba tangu kuanza mashambulizi ndege za NATO zimekwisha wamalizia maisha raia 718 wasiokuwa na hatia.

Helicopta ya Ufaransa inayo tumiwa kwa mashambulzi ya NATO nchini Libya
Helicopta ya Ufaransa inayo tumiwa kwa mashambulzi ya NATO nchini Libya AFP / Alexander Klein
Matangazo ya kibiashara

Muda mchache baada ya NATO kuendesha mashambuliz mapya mjini Tripoli, ma balozi wa nchi za NATO katika mkutano wao mjini Brussels Ubelgiji wamekubaliana kuviruhusu vikosi hivyo kuzidi kuendesha hujuma nchini Libya kwa siku 90 zijazo hadi septemba.

Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema ” huu ni ujumbe nyeti kwa utawala wa Gadaffi kwamba tumepania kuendeleza harakati za kuwalinda raia wa libya”.

“Tutaendeleza juhudi zetu ili kutekeleza kupengele la Umoja wa mataifa kinachoagiza kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya Gadaffi, ameongeza kuwa tutazidisha harakati zetu hadi pale tutapomuona Gadaffi anaondoka”

NATO ambayo kampeni yake nchini Libya ingelimalzika jUNI 27, imezidisha mashambulizi ya anga wiki hizi mbili za nyuma kwa kushambulia maeneo kadhaa mjini Tripoli na kumzima Gadaffi kuendesha mashambulizi dhidi ya uasi ulianza mwezi Februari.

Uamuzi huo unatowa muda kwa mataifa uanachama wa NATO kutathmini na kuandaa michango katika kipindi hicho cha siku 90. amesema hivyo mwanadiplomasia moja wa NATO. Na kuongeza kuwa kumekuwa na ishara chanya ya kupanua rasiliamali kubwa”

Serikali ya Libya ilitangaza jumanne kuwa tangu machi 19 hadi mei 26, watu 718 wamekwisha fariki huku watu 4067 wakijeruhiwa, 433 wakiwa katika hali mahtuti. Msemaji wa serikali ya libya moussa Ibrahim amesema kuwa idadi hiyo ni kwa mujibu wa wizara ya afya. Ni vigumu sana kuchunguza aidha kuthibitisha idadi hiyo. Msemaji huyo wa serikali ya Libya amesema kwamba idadi hiyo ni ya raia wa kawaida, idadi ya wanajeshi haijafahamishwa na wizara ya ulinzi.

NATO imetupilia mbali idsdi hiyo na kusema kwamba ni vigumu kuchunguza idadi hiyo kwa kuwa vikosi vya NATO havina wanajeshi ardhini, bali NATO imekuwa ikiendesha operesheni za anga ili kutekeleza kipengele cha Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano na vyombo vya habari mjini Tripoli msemaji wa serikali ya Gadaffi amesema kwamba kuondoka kwa Gadaffi nchini kama inayodaiwa na NATO pamoja na kundu la G8 inaweza kusababisha madhara makubwa. Amesema “Gadaffi akiondoka usalama utatoweka kabisa”

Ibrahim amekanusha habari kwamba rais wa afrika kusini Jacob zuma amejadili na Gadaffi walipokutana siku ya jumatatu kuhusu kuondoka kwake. Zuma hakuongea kamwe na rais Gadaffi kuhusu hilo.

Awali rais Zuma alifahamisha kuwa Kanali Gadaffi alikataa kuondoka Libya licha ya jamii ya kimataifa kumtaka aondoke nchini humo na mashambulizi ya NATO yaendelea kuishambulia serikali yake.

Kanali Gadaffi alitangaza na kuomba usitishwaji mapigano ili kuruhusu mjadiliano ya raia wa libya na kuthibitisha kuwa hayupo tayari kuondoka nchini mwake licha ya matatizo yanayo mkumba wakati huu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.