Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI

Waasi wa Libya wasaka kutambuliwa na Marekani

Waasi wa Libya wakiongozwa na Mahmud Jibril wanaendelea na mkakati wao wakutaka kutambuliwa kama Utawala kamili baada ya Uingereza kuikubalia kufungua Ubalozi nchini humo sasa wanaiomba Marekani nayo iwape fursa hiyo.

Reuters/Andrew Winning
Matangazo ya kibiashara

Jibril anatarajiwa kuelekea Ikulu ya Marekani White House kwa ajili ya kusaka uungwaji mkono baada ya kufanikiwa kuutwaa Uwanja wa Ndege wa Misurata kutoka kwa vikosi vya Kanali Muammar Gaddafi.

Jibril ambaye anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Baraza la Taifa la Mabadiliko nchini Libya NTC atakutana na Mshauri wa Ulinzi wa Marekani Tom Donilon.

Maofisa wa Serikali ya Marekani hawajasema iwapo Jibril atapata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama atakapozuru White House baadaye Ijumaa kusaka uungwaji mkono wa Kidiplomasia.

Waasi ambao wameweka makazi katika eneo la Kaskazini mwa Jiji la Benghazi wanapigana kuitaka Washington iweze kuwatambua kama watawala halali wa nchi ya Libya.

Hadi sasa ni Ufaransa, Italia, Gambia na Qatar ndiyo wanawatambua NTC lakini Marekani bado haijatoa kauli ya kufanya hivyo huku Jibril akisema wakati wowote Jordan wanaweza kuwatambua.

Jibril amesema lengo lao ni kuitaka dunia kutambua kile ambacho wanakifanya na hivyo waweze kuwaunga mkono na kupata uhalali wa kuwa utalawa kamili katika nchi ya Libya.

Nazo taarifa kutoka Benghazi zinaeleza Mkandarasi Binafsi raia wa Ufaransa wameuawa na wenzake wanne wamekamatwa wakati wakitaka kuingia kwenye mji huo ambao makazi ya waasi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ufaransa Bernard Valero amethibitisha hilo na kuongeza tukio hilo limetokea kwenye kituo cha ukaguzi.

Katika hatua nyingine serikali ya Kanali Gaddafi kupitia Msemaji wake Mussa Ibrahim imethibitisha vifo vya watu watatu vilivyosababishwa na mashambulizi ya Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO.

00:13

Mussa Ibrahim Msemaji wa Serikali ya Libya Akithibitisha Mashambulizi ya NATO

Ibrahim amewaambia wanahabari mashambulizi hayo ambayo yalikuwa yanalenga makazi ya Kanali Gaddafi yamesababaisha vifo hivyo baada ya NATO kutumia roketi.

Nayo Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ICC inatarajia kutoa waranti ya kukamatwa kwa Kanali Gaddafi mwishoni mwa mwezi huu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Franco Frattini amenukuliwa.

Frattini amesema waranti hiyo itakuwa ni hatua kubwa katika kufanikisha kuuangusha Utawala wa Kanali Gaddafi ambaye atashindwa kuishi uhamisho kwa kuhofia waranti hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.