Pata taarifa kuu
SYRIA

Ban Ki-moon ataka matumizi ya nguvu yasitishwe nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amemtaka Rais wa Syria Bahar Al Assad kuacha kutumia nguvu katika kuzima maandamano yanayoendelea katika nchi yake na badala yake asikilize mwito wa mabadiliko unaotolewa na wananchi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa UN Ban amewaambia wanahabari huu ni wakati wa Rais Assad kusikiliza kilio cha kufanya mabadiliko na kuacha mara moja kutumia silaha kuzima maandamabo ya amani ambayo yanafanyika katika taifa hilo.

Maneno ya Ban yanakuja baada ya wanaharakati kusema serikali ya Syria imezidi kuimarisha ulinzi katika Miji ya Banias, Homs na Daraa huku wakitumia vifaru kuwasambaratisha waandamanaji ambao wamekataa kutii amri ya kurudi majumbani mwao.

Katibu Mkuu wa UN ameongeza kuwa ameshafanya mazungumzo mara kwa mara na Rais Assad lakini hajaona utekelezaji wa kile ambacho wamekiongea na badala yake nguvu za kijeshi zimeongezwa kudhibiti maandamano.

Katika hatua nyingine Ban amekiri kukatishwa tamaa kutokana na wafanyakazi wake kuzuiliwa kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wananchi ambao wanahitaji huduma ya haraka baada ya kutokea kwa mashambulizi.

Ban amesema waliruhusiwa kupeleka misaada ya kibinadamu kuanzia tarehe 5 ya mwezi May katika eneo la Kusini wa Jiji la Daraa lakini zoezi hilo limekuwa gumu kutokana na kukatwa kwa mawasiliano katika sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Nao Umoja wa Ulaya EU unatarajiwa kuweka vikwazo vipya kwa nchi ya Syria baadaye juma hili huku swali kubwa likiwa ni kwa nini jina la Rais Assad halipo katika orodha ya watu 13 waliowekewa vikwazo vya kusafiri pamoja na kuzuiliwa kwa mali zao.

Mkuu wa Sera za Kimataifa katika EU Catherine Ashton amewaambia wabunge wa Bunge la Ulaya jina hilo halijaweka kwa kuwa wameanza na watu hao 13 na kisha wataendelea kuongeza kwa kadri itakavyokuwa.

00:52

Catherine Ashton - Mkuu wa Sera za Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya EU

Ashton amesema kwa kuwa baadaye juma hili watakutana itakuwa ni nafasi nzuri ya kuamua iwapo jina hilo liongezwe kwenye orodha hiyo au lisiwepo pamoja na kuangalia vikwazo zingine ambavyo vinastahili kwa nchi hiyo.

Syria imeendelea kutishia itakumbana na vikwazo vikali zaidi iwapo itaendelea na hatua ya kuwashambulia waandamanaji wa amani huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle akisema hakuna utani katika hilo.

Tangu kuanza kwa machafuko nchini Syria watu wanaokadiriwa kufikia mia saba wanataja kupoteza maisha huku wengine maelfu wakishikiliwa na polisi kutokana na kushiriki kwenye maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.