Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-MAPIGANO-USALAMA

Maombolezo na vurugu mashariki mwa Ukraine

Ukraine inaomboleza leo Alhamisi Januari 15, hatua iliyochukuliwa na rais Petro Poroshenko baada ya vifo vya raia 12 waliouawa Jumanne wiki hii katika shambulio la roketi dhidi ya basi karibu na mji wa Donetsk.

Shambulio dhidi ya basi la raia katika mji wa Volnovakha, nchini Ukraine ambalo liligharimu maisha ya watu wengi.
Shambulio dhidi ya basi la raia katika mji wa Volnovakha, nchini Ukraine ambalo liligharimu maisha ya watu wengi. REUTERS/Ukraine's Ministry of Internal Affairs
Matangazo ya kibiashara

Mapigano mashariki mwa Ukraine yameongezeka tangu lilipotolewa tangazo la mkataba wa kusitisha mapiganao uliosainiwa Desemba 9 mwaka 2014. Ujumbe wa uangalizi wa OSCEumeelezea wasiwasi wake, na rais Ukraine ametangaza kutumwa kwa wanajeshi 50,000 wa ziada.

Vurugu zimeongezeka na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ukraine na Urusi umeendelea kuingiliwa na utata. Siku ya Jumatatu, mawaziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Urusi, Ujerumani na Ufaransa, ambao wamekutana mjini Berlin, wameshindwa kukubaliana juu ya tarehe ya mkutano huo kwa ajili ya Ukraine, utakaofanyika nchini Kazakhstan.

Jumanne shambulio dhidi ya basi la raia katika mji wa Volnovakha, hali hiyo imesababisha hali ya sintofahamu nchini Ukraine. Hili ni shambulio lililosababisha maafa makubwa tangu miezi minne iliyopita.

Waangalizi wa OSCE waliwasili haraka katika eneo la tukio. OSCE inatiwa wasiwasi kuhusu ongezeko la machafuko, kama alivyoeleza mmoja wa wasemaji mashariki mwa Ukraine, Laurence Couture-Gagnon.

"Uchunguzi wa pamoja unapaswa kufanyika na viogozi tawala. Tunajaribu kukusanya vithibitisho. Tunatiwa wasiwasi sana kuhusu hali na kuongezeka kwa vurugu katika siku za karibuni", amesema Couture-Gagnon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.