Mataifa makubwa yasusia mafunzo ya Sri Lanka ya kukabiliana na ugaidi
Mataifa matano yenye nguvu duniani, yamesusia semina ya namna ya kupambana na ugaidi iliyoandaliwa na serikali ya Sri Lanka kwa madia kuwa, nchi hiyo ilihusika katika mauaji ya raia wakati wa oparesheni ya kulitokomeza kundi la Tamil Tigers.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Miongoni mwa mataifa yaliyokataa kushiriki katika semina hiyo ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujapan ambazo zote kwa pamoja zimeitaka serikali ya nchi hiyo kuchunguza kwa kina mauaji ya raia.
Taarifa kutoka katika waandaaji hao, inapasha kuwa serikali ya Sri Lanka, ilifanikiwa kuwashinda waasi hao, kutokana na kujifunza kwa miaka mingi jinsi ya kupambana na wavamizi, sanjari na utayari thabiti wa kisiasa pamoja na kuungwa mkono.