Pata taarifa kuu

Haiti: Kutokuwa na uhakika kuhusu muundo wa baraza la mpito la rais

Nchini Haiti, vyama vya kisiasa na mashirika ya kiraia kimsingi yalikuwa na hadi Jumatano Machi 13 jioni kuwasilisha kwa Jumuiya ya Caribbean majina ya watu walioteuliwa kuwa wajumbe wa baraza la mpito la rais la siku zijazo. Baraza hili litakuwa na jukumu la kuteua mkuu mpya wa serikali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Rais wa Guyana Irfaan Ali na Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness wanahudhuria mkutano wa dharura kuhusu Haiti wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Caribbean mjini Kingston, Jamaica, Machi 11, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Rais wa Guyana Irfaan Ali na Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness wanahudhuria mkutano wa dharura kuhusu Haiti wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Caribbean mjini Kingston, Jamaica, Machi 11, 2024. © Andrew Caballero-Reynolds / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Huko Haiti, kwa sasa hakuna mawasiliano rasmi kutoka kwa Caricom, ambayo ina jukumu la mpatanishi. Na kama baadhi ya vyombo vya habari vya Haiti vilithibitisha, kufikia Jumatano jioni, majina yalikuwa yalitumwa kwa jumuiya ya Caribbean ndani ya muda uliowekwa, ni vyema, katika hatua hii, kuzungumzia uvumi kuhusu muundo wa baraza hili la rais la siku zijazo.

Baadhi ya vyama vya siasa au mashirika ya kiraia, yaliyohojiwa na RFI, yanathibitisha kuwa yamewasilisha jina la mtu binafsi. Pia inafahamika kwamba wengine wamepuuzilia mbali mchakato huu, ingawa walikuwa wameteuliwa kuwa sehemu yake.

Mchakato mgumu

Habari Nyingine: wakati jina moja tu liliombwa kwa kila shirika au chama, kundi, lile la Desemba 21, ambalo lilitia saini makubaliano mnamo mwaka 2022 na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Ariel Henry, liliwasilisha kwa Caricom majina ya watu kadhaa. Ishara ya wazi ya malumbano ya ndani.

Na hilo ndilo tunalohitaji kukumbuka. Mchakato huu mgumu sana unaonyesha mivutano na udhaifu wa vyombo hivi vinavyotofautiana kabisa. Iwapo baraza hili la rais litaundwa, mtu hujiuliza itakuwaje basi kukubali kumteua Waziri Mkuu, kama ilivyopangwa kikanuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.