Pata taarifa kuu

Kenya kuendelea na mpango wa kutuma polisi Haiti licha ya waziri mkuu kujiuzulu

Nairobi – Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amejiuzulu baada ya wiki kadhaa za machafuko yanayoongozwa na magenge ya watu wanaotaka aondolewe madarakani.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry. AP - Andrew Kasuku
Matangazo ya kibiashara

Henry alikuwa nchini Kenya kutia saini mkataba wa kutumwa kwa kikosi cha polisi wa kimataifa kusaidia kukabiliana na ghasia wakati makundi wa magenge yaliposhambulia vituo vya polisi na kuvamia magereza mawili makubwa zaidi ya Haiti.

Ndege iliyokuwa imembeba Henry ilizuiwa kutua kufuatia mashambulio ya magenge katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haiti.

Magenge yenye silaha yamekuwa yakishinikiza waziri mkuu wa Haiti kujiuuzulu.  (AP Photo/Odelyn Joseph)
Magenge yenye silaha yamekuwa yakishinikiza waziri mkuu wa Haiti kujiuuzulu. (AP Photo/Odelyn Joseph) AP - Odelyn Joseph

Marekani imetangaza kutoa msaada zaidi wa kifedha kwa Haiti, kufanikisha kikosi cha kimataifa, kitakachoongozwa na polisi kutoka nchini Kenya, kusaidia kukabiliana na magenge yenye silaha, yanayoendelea kusababisha utovu wa usalama nchini humo.

Hili limethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Antony Blinken, wakati alipohudhuria kongamano la Kimataifa jijini Kingstone Jamaica, kujadili hali inavyoendelea Haiti.

Marekani imesema inaunga mkono kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya
Marekani imesema inaunga mkono kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya AFP - ANDREW CABALLERO-REYNOLDS

Haya yanajiri wakati huu serikali ya Kenya ikiwa imesisitiza kuendelea na mpango wake wa kuwatuma maofisa wa polisi nchini Haiti licha ya kuongezeka kwa ghasia za magenge katika nchi hiyo ya Caribbean.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya  Kithure Kindiki hapo jana Jumatatu,  mpango wa kutumwa kwa polisi hao elfu moja umefikia katika hatua za mwisho.

Waziri Kindiki pia alisema kuwa sheria za utekelezaji, kama vile kuzuiliwa na kukamatwa, zimekamilika.

Kenya inalenga kuwatuma polisi elfu moja nchini Haiti kusaidia kupambana na magenge yenye silaha.
Kenya inalenga kuwatuma polisi elfu moja nchini Haiti kusaidia kupambana na magenge yenye silaha. AP - Stringer

Aidha waziri Kindiki alisema kuwa serikali ya Kenya imeshughulikia masuala yote yaliyoibuliwa mahakamani ambayo yalikuwa yamezuia utekelezwaji wa mapngo huo.

Licha ya tangazo hilo la serikali, tarehe kamili ambayo maafisa hao wataondoka nchini nchini Kenya bado haijaekwa wazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.