Pata taarifa kuu

Marekani: Mahakama ya Juu kushughulikia suala la kinga ya uhalifu ya Trump

Mahakama ya juu kabisa ya Marekani ilitangaza Jumatano hii kwamba imekubali kujibu swali la kinga ya uhalifu ya Donald Trump kama rais wa zamani. Mijadala hiyo itafanyika “wiki ya Aprili 22.

Donald Trump anasubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi katika mahakama ya New York, Alhamisi Februari 15, 2024.
Donald Trump anasubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi katika mahakama ya New York, Alhamisi Februari 15, 2024. © Jefferson Siegelon Siegel / AP
Matangazo ya kibiashara

Je, Donald Trump atanufaika na "kinga kabisa" kwa matendo yake aliyoyafanya wakati wa muhula wake kama Rais wa Marekani, kama utetezi wake unavyosisitiza? Hili ndilo swali ambalo Mahakama ya Juu ya Marekani ilikubali kushughulikia Jumatano hii.

Katika taarifa ambayo haijatiwa saini, mahakama ya juu zaidi ya taifa inasema itazingatia "ikiwa na, kwa kiwango gani rais wa zamani ananufaika na kinga ya rais dhidi ya kufunguliwa mashitaka ya jinai kwa mwenendo unaodaiwa kuhusisha vitendo rasmi wakati wa mamlaka yake".

Kuzidisha rufaa

Kesi ya rais huyo wa zamani wa chama cha Republican, kwa majaribio haramu ya kutengua matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Joe Biden, awali ilipangwa kuanza Machi 4.

Lakini mtu anayepewanafsi kubwa ya kushinda katika kura za mchujo za chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa Novemba anataka, kupitia rufaa zake nyingi, kufikishwa mahakamani akiwa amechelewa iwezekanavyo, angalau baada ya uchaguzi wa urais. Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka manne tofauti ya jinai.

Lakini utaratibu mzima ulisitishwa huku suala la kinga ya uhalifu lililodaiwa na Donald Trump likiamuliwa na mahakama. Mnamo Februari 6, mahakama ya Rufaa ya shirikisho iliondoa kinga hii ya uhalifu. Kwa hivyo Donald Trump aligeukia Mahakama ya Juu ili kusimamishwa kwa kuanza kutumika kwa uamuzi huu.

Mashtaka manne ya jinai

Hivyo, kwa kukubali kuchukua hatua, Mahakama ya Juu kwa kiasi fulani inamridhisha Donald Trump kwa kutoruhusu uamuzi wa rufaa kuanza kutumika hadi itakapofanya uamuzi wake yenyewe. Lakini kwa kuamua kujadili mwezi wa Aprili, makataa mafupi, pia imekubali ombi la mwendesha mashtaka maalum Jack Smith ambaye anataka Mahakama, ikiwa inaangalia swali hilo, kufanya hivyo kwa njia ya haraka.

Lakini wachambuzi wengi wa masuala ya kisheria na kisiasa walisema Jumatano jioni kwamba ilikuwa mafanikio kwa mkakati wa kuchelewesha wa Donald Trump, kwani uamuzi wa Mahakama ya Juu unapunguza zaidi uwezekano wa kesi hiyo kufanyika kabla ya uchaguzi wa urais, hata kama majaji tisa walikataa kinga yake. Iwapo atachaguliwa tena, mara alipozinduliwa Januari 2025, anaweza kuamuru kusitishwa kwa kesi za shirikisho dhidi yake.

Trump aliondolewa kwenye mchujo wa chama cha Republican huko Illinois

Baada ya Maine na Colorado, siku ya Jumatano, jaji wa Illinois kumtangaza Donald Trump kuwa hastahili kutokana na matendo yake wakati wa kuvamiwa kwa Capitol na kuamuru kuondolewa kwa kura kwa jina lake wakati wa mchujo huo wa Republican. Tracie Porter, Mdemokrat, alisema rais huyo wa zamani lazima aondolewe kwenye kura za mchujo wa Illinois kwa chama cha Republican, ambao umepangwa kufanyika Machi 19, "au ahakikishe kuwa kura zilizopigwa kwake zimefutwa".

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.