Pata taarifa kuu

Marekani: Mkuu wa Pentagon amelazwa hospitalini kwa saratani ya kibofu

Mkuu wa Pentagon Lloyd Austin, ambaye kulazwa kwake hospitalini hivi majuzi kuliwekwa wazi kwa kuchelewa, na kusababisha utata, anatibiwa saratani ya kibofu, madaktari walitangaza Jumanne hii, Januari 9, wakinukuliwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani.

Lloyd Austin alificha kulazwa kwake hospitalini kwa saratani ya kibofu.
Lloyd Austin alificha kulazwa kwake hospitalini kwa saratani ya kibofu. © Cliff Owen / AP
Matangazo ya kibiashara

"Saratani yake ya kibofu iligunduliwa mapema na anaendelea vizuri," Madaktari wake wallihakikisha katika taarifa ya Pentagon.

Kulazwa kwake hospitalini kuliwekwa wazi siku nne baadaye

Kulazwa hospitalini kwa mkuu wa Pentagon tangu Jumatatu Januari 1 kwa matatizo ya kiafya kuliwekwa wazi siku nne tu baadaye na Wizara ya Ulinzi, kinyume na itifaki, na kuzua ukosoaji kutoka kwa chama cha waandishi wa habari wa Pentagon.

Tarehe ya kuruhusiwa kuondoka kwake hospitali bado haijajulikana, amebainisha msemaji wa Wizara ya Ulinzi, akithibitisha kwamba Lloyd Austin hata hivyo alikuwa ameanza tena "kazi zake" tangu Ijumaa ya wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.