Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa Urais nchini Venezuela: Nicolas Maduro hajui kama atakuwa mgombea

Waangalizi wengi na wafuasi wake wanaona Nicolas Maduro kama mgombea, lakini bado hajajua kama atawania karika uchaguzi wa urais. Siku ya Jumatatu Rais wa Venezuela alihakikisha, wakati wa mahojiano ya televisheni, kwamba hajui kama atawania urais kwa muhula wa tatu.

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akionyesha kura yake wakati wa kura ya maoni ya uchaguzi kuhusu haki za Venezuela kwa eneo linaloweza kuwa na utajiri wa mafuta la Esequiba, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na mzozo wa mpaka kati ya Venezuela na Guyana, huko Caracas, Venezuela, Desemba 3, 2023.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akionyesha kura yake wakati wa kura ya maoni ya uchaguzi kuhusu haki za Venezuela kwa eneo linaloweza kuwa na utajiri wa mafuta la Esequiba, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na mzozo wa mpaka kati ya Venezuela na Guyana, huko Caracas, Venezuela, Desemba 3, 2023. © Leonardo Fernandez Viloria / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Bado ni mapema. Mwaka ndio unaanza sasa. Mungu pekee ndiye anajua. Sio Diosdado (Diosdado Cabello), Mungu. Wacha tungoje kitakachotokea katika uchaguzi (...) Nina hakika kwamba kwa baraka za Mungu tutafanya uamuzi bora zaidi," alisema, akijaribu kulinganisha maneno kati ya Mungu na Makamu wa Rais wa zamani Diosdado ( Dieudonné) Cabello mara nyingi alichukuliwa kuwa nambari 2 katika utawala wa Venezuela.

Diosdado Cabello, makamu wa rais wa sasa wa chama cha United Socialist Party of Venezuela (PSUV) tayari amesema mara kadhaa kwamba PSUV ina mgombea wake: Nicolas Maduro. Mgombea huyo wa utawala atakabiliana na aliyekuwa mbunge Maria Corina Machado ndani ya kipindi cha miezi sita mwaka huu wa 2024 (tarehe itapangwa), ambaye alishinda kwa urahisi kura za mchujo na aliweza kuwaleta pamoja vigogo wengi nyuma yake.

Kwa sasa hana haki ya kuwani katika uchaguzi huo lakini aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu kama sehemu ya mazungumzo kati ya serikali na upinzani. Maria Corina Machado aliwekewa vikwazo kwa miaka kumi na mitano ya kutostahiki uchaguzi wowote kutokana na madai ya ufisadi na uhaini kwa sababu aliunga mkono vikwazo vya Marekani dhidi ya Venezuela. Washington imeendelea kurejelea msimamo wake kwamba kufutwa kwa hatua inayomzuia Maria Corina Machado kuwania uchaguzi wa urais ni mojawapo ya masharti ya kuondolewa kwa vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.