Pata taarifa kuu

Marekani: Mfungwa ashtakiwa kwa kumchoma kisu muuaji wa George Floyd mara 22

Mfungwa mmoja ameshtakiwa kwa jaribio la kuua kwa kumchoma kisu Derek Chauvin mara 22 wiki iliyopita, afisa wa polisi aliyemuua Mmarekani mwusi George Floyd, katika gereza la shirikisho, waendesha mashtaka wametangaza.

Derek Chauvin  alipatikana na hatia ya mauaji na mahakama ya jimbo la Minnesota kufuatia kesi iliyofuatwa kwa karibu mwaka wa 2021.
Derek Chauvin alipatikana na hatia ya mauaji na mahakama ya jimbo la Minnesota kufuatia kesi iliyofuatwa kwa karibu mwaka wa 2021. Pool via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Kifo cha George Floyd, Mei 2020 wakati wa kukamatwa kwake, kilichochea maandamano makubwa yaa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani na nje ya mipaka ya Marekani. Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu wakati huo alikuwa afisa mkongwe wa vikosi vya usalama huko Minneapolis (kaskazini), alionekana akipiga goti kwenye shingo la George Floyd, 46, kwa dakika kadhaa huku Floyd akisikika akisema kuwa hawezi kupumua.

Akitumikia kifungo cha miaka 22 na nusu jela, Bw. Chauvin, 47, alishambuliwa mnamo Novemba 24, 2023 katika maktaba ya gereza la shirikisho huko Tucson, Arizona. Alinusurika majeraha yake.

Mmoja wa wafungwa wenzake, John Turscak, 52, anashtakiwa kwa kumdunga kisu zaidi ya mara 20 kwa kutumia kisu cha kujitengenezea nyumbani, kulingana na hati ya mahakama.

Mtu huyo aliwaambia wachunguzi kwamba alichagua kwa makusudi tarehe ya shambulio hilo, siku ya "Black Friday", maarufu kwa punguzo la kibiashara, akimaanisha vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi "Black Lives Matter", kwa mujibu wa chanzo hicho.

“Bwana Turscak aliwaambia maafisa wa magereza kwamba angemuua (Bw. Chauvin) ikiwa hawangechukua hatua ya haraka,” hati hiyo yaendelea.

Ofisi ya waendesha mashtaka wa shirikisho huko Tucson ilisema kuwa imemshtaki Bw. Turscack kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kujaribu kuua, kuadhibiwa kwa hadi miaka 20 jela, na shambulio lililosababisha majeraha mabaya. Mwanamume huyo pia anadaiwa kumchoma mfungwa mwingine zaidi ya mara 20, tena kwa kisu.

Ingawa hakuna taarifa kwa vyombo vya habari au malalamiko yanayotoa jina kamili la Bw. Chauvin, chanzo rasmi kimethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba mwathiriwa alikuwa afisa wa polisi wa zamani wa Minneapolis.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu hali yake ya afya kwa sasa.

Kifo cha George Floyd kilizusha maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi na ghasia za polisi.

Kulingana na tukio la mauaji hayo lililorekodiwa na kurushwa mtandaoni, Derek Chauvin alikuwa ameweka goti lake kwenye shingo la George Floyd, hata mara tu kijana huyo mweusi mwenye umri wa miaka arobaini alipozirai na mapigo yake ya moyo kutoonekana. Maafisa wengine wawili wa polisi walisaidia kumshikilia.

Alipatikana na hatia ya mauaji na mahakama ya jimbo la Minnesota kufuatia kesi iliyofuatwa kwa karibu mwaka wa 2021.

Mahakama ya Juu ya Marekani ilikataa rufaa ya Derek Chauvin dhidi ya hukumu hii mwezi Novemba.

Afisa huyo wa zamani wa polisi aliomba kubatilishwa kwa hukumu hiyo, kwa misingi kwamba utangazaji uliokithiri wa vyombo vya habari wa kesi hiyo na hatari ya ghasia kumemnyima kesi "ya haki".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.