Pata taarifa kuu

Marekani yaidhinisha dawa ya Zepbound dhidi ya tatizo la unene uliopindukia

Dawa hiyo kutoka kwa kampuni ya Kimarekani Eli Lilly itatumiwa kwa sindano ya kila wiki. Molekuli iliyotumiwa ilikuwa tayari imeidhinishwa dhidi ya ugonjwa wa kisukari.

Mmoja kati ya watu kumi wana tataizo la unene uliopindukia duniani, mara tatu zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Mmoja kati ya watu kumi wana tataizo la unene uliopindukia duniani, mara tatu zaidi ya miaka 50 iliyopita. © Shutterstock/Fuss Sergey
Matangazo ya kibiashara

Ni dawa ambayo inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu wanene nchini Marekani. Mamlaka ya afya ya Marekani imetangaza kwamba waliidhinisha Jumatano Novemba 8 dawa inayotarajiwa dhidi ya unene kupita kiasi kutoka kwa kampuni ya Kimarekani Eli Lilly, mshiriki wa hivi punde katika soko ambalo limekuwa kubwa kwa tasnia ya dawa. Matibabu, ambayo yatauzwa kwa jina la Zepbound nchini Marekani, yatatumiwa kwa sindano mara moja kwa wiki.

Molekuli iliyotumiwa tayari imeidhinishwa dhidi ya ugonjwa wa kisukari, lakini wakati mwingine imeagizwa nje ya mapendekezo rasmi na baadhi ya madaktari kwa kupoteza uzito, kutokana na ufanisi wake. Katika jaribio kubwa la kimatibabu, Zepbound ilionyeshwa kupunguza uzito, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) imesema katika taarifa.

"Unene na uzito kupita kiasi ni matatizo makubwa ya afya, ambayo yanaweza kuhusishwa na baadhi ya sababu kuu za kifo, kama vile ugonjwa wa moyo na mishipa, kiharusi au kisukari," amesema John Sharretts, mkurugenzi wa tawi linalojitolea kwa unene uliopindikia katika FDA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.