Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Kesi ya kihistoria ya Trump itaanza Machi 4, 2024

Kesi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump itasikilizwa kuanzia Machi 4, 2024 katika mahakama ya shirikisho mjini Washington kwa majaribio yake ya kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020, katikati ya kampeni ya kuwania kiti cha urais.

Aliyekuwa Rais wa Marekani na mgombea katika kura za mchujo za chama cha Republican Donald Trump mnamo Agosti 12, 2023 huko Iowa.
Aliyekuwa Rais wa Marekani na mgombea katika kura za mchujo za chama cha Republican Donald Trump mnamo Agosti 12, 2023 huko Iowa. © EVELYN HOCKSTEIN / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jaji Tanya Chutkan, ambaye ataongoza kesi hiyo, alitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu Agosti 28 wakati wa kikao kilichohusu mapendekezo ya pande hizo mbili.

Mwendesha Mashtaka Maalum Jack Smith alitaka kesi ya Donald Trump huko Washington ianze Januari 2, 2024, lakini Jaji Tanya Chutkan amesema ni muda mfupi sana kujitayarisha, huku upande wa utetezi ukitaka kusogezwa mbele, mwezi Aprili, "mbali na inavyohitajika", kulingana na kwa Jaji Tanya Chutkan.

Tarehe hii si ya haraka, aliongeza jaji, akisisitiza kwamba kesi hiyo itafunguliwa kwa muda wa miaka mitatu, miezi miwili na siku sita baada ya Januari 6, 2021. Alikuwa akizungumzia shambulio la Capitol, makao makuu ya Baraza la Congress, na mamia ya wafuasi wa Donald Trump waliovamia jengo la vikao vya Wawakilishi kuzuia kuthibitishwa kwa ushindi wa mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden.

Kwa hivyo hii itakuwa kesi ya kwanza ya jinai kwa mtu anayepewa nafasi kubwa kushinda kura za mchujo za chma cha Republican, ambaye pia atahukumiwa kuanzia mwisho wa mwezi Machi 2024 katika Jimbo la New York kwa malipo ya kutiliwa shaka kwa mwigizaji wa zamani wa filamu za X, Mei 2024 na mahakama huko Florida (kusini mashariki) kwa usimamizi wake wa uzembe wa nyaraka za siri baada ya kuondoka Ikulu.

Tarehe ya kusikilizwa kwa kesi yake katika kesi ya nne, ile ya shinikizo la uchaguzi nchini Georgia mwaka 2020, mashitaka ambayo yalimfanya apigwe picha ya rekodi za kumbukumbu wiki iliyopita, ambalo ni tukio la kihistoria la rais wa zamani, bado haijatangazwa.

'Uhalifu wa Kihistoria'

Bila ya kustaajabisha, Jaji Chutkan alipuuzilia mbali hoja nyingi za utetezi, ambazo zilidai miaka miwili na nusu, sawa na muda wa uchunguzi, kuchunguza nyaraka za mashtaka.

Wakili wa Donald Trump, John Lauro, alikashifu vikali tarehe iliyopendekezwa na mwendesha mashitaka Januari 2024. "Unaomba kesi isikilizwe, sio kesi ya haraka," aliwaambia majaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.