Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Ecuador: Fernando Villavicencio, mmoja wa wagombea 8 katika uchaguzi wa urais auawa

Mmoja wa wagombea wanane wa uchaguzi wa urais wa Agosti 20, 2023 aliuawa na mshambuliaji Jumatano usiku Agosti 9 kaskazini mwa Quito. Rais wa zamani wa tume ya udhibiti wa bunge ambapo alishutumu ufisadi wa mwanachama wa utawala wa zamani wa Rafael Correa, Fernando Villavicencio hivi majuzi alilishutumu kundi la Sinaloa na wapinzani wa kisiasa kwa kutaka kumuua.

Watu wakijificha baada ya milio ya risasi zilizomuu mgombea urais nchini Ecuador Fernando Villavicencio mjini Quito mnamo Agosti 9, 2023.
Watu wakijificha baada ya milio ya risasi zilizomuu mgombea urais nchini Ecuador Fernando Villavicencio mjini Quito mnamo Agosti 9, 2023. AFP - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Quito, Éric Samson

Fernando Villavicencio alikuwa akitoka kwenye mkutano wa kisiasa aliposhambuliwa, baada tu ya kuingia kwenye gari lake. Video iliyosambazwa kwenye mitandao yote ya kijamii inamuonyesha akiwa amezungukwa na walinzi, mafisa wa polisi na askari upande wa kulia wa gari, lakini inaonekana muuaji au wauaji walivamia kutoka upande wa kushoto wa gari ambao haukuwa na ulinzi hata kidogo.

Wasiwasi

Hofu iliwashika mara moja wale wote waliokuwepo ambao walikimbilia nyuma ya magari au katika jengo ambalo mkutano wa kisiasa ulikuwa umemalizika.

Akiwa na umri wa miaka 59, mwanaharakati wa zamani wa chama cha wafanyakazi wa mafuta, mwandishi wa habari na mbunge, Fernando Villavicencio alisafirishwa hadi Kliniki ya wanawake iliyo karibu ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Juán Zapata na kisha mjomba wake Galo Valencia walithibitisha kifo chake. Kulingana na kura za hivi punde, Fernando Villavicencio alishika nafasi ya pili katika nia ya kupiga kura kwa karibu 13% kulingana na taasisi ya Cedatos, nyuma ya wakili Luisa Gonzalez (26.6%), mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa mrengo wa kushoto Rafael Correa.

Makundi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya yahusishwa

Fernando Villavicencio hivi majuzi alikuwa ameshutumu shirika la Sinaloa na washirika wa karibu wa rais wa zamani Rafael Correa kwa kutaka kumuua kwa kuhofia mpango wake wa uchaguzi ambao ulipanga ujenzi wa gereza lenye ulinzi mkali kwa walanguzi wakuu wa dawa za kulevya pamoja na kuundwa kwa kitengo cha polisi wasomi ili kukabiliana na makundi hayo.

Mshambuliaji alikamatwa lakini hakunusurika, kulingana na Idara ya Sheria. "Uhalifu wa kupangwa umeenda mbali sana, wahusika watakamatwa," amesema Rais Guillermo Lasso kabla ya kuitisha kwa dharura mkutano wa maafisa wakuu wa usalama nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.