Pata taarifa kuu

Uavyaji mimba nchini Marekani: Warepublican washindwa tena Ohio

Wapiga kura katika jimbo la Ohio Jumanne wamekataa mageuzi ya kikatiba ya ndani ambayo yangefanya iwe vigumu kuandaa na kupitisha kura za maoni. Warepublican, ambao wanahusika katika kuandaa nakala hii , walitaka kufanya ushindi kwa kambi inayounga mkono uavyaji mimba kuwa ngumu zaidi. Lakini walishindwa tena, kama kura nyingine za hivi majuzi kuhusu suala la uavyaji mimba nchini Marekani.

Wapiga kura wa Ohio Jumanne walikataa mageuzi ya katiba ya eneo hilo ambayo yangefanya iwe vigumu kuandaa na kupitisha kura za maoni.
Wapiga kura wa Ohio Jumanne walikataa mageuzi ya katiba ya eneo hilo ambayo yangefanya iwe vigumu kuandaa na kupitisha kura za maoni. © Megan Jelinge, Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa jimbo la Ohio wamefutilia mbali mnamo Jumanne  mageuzi madhubuti ya ufikiaji wa utoaji mimba katika jimbo hilo la Marekani, ushindi kwa wanaharakati wanaopendelea haki ya kutoa mimba na kushindwa kwingine kwa Warepublican, ambao hivi majuzi waliweka vikwazo kwenye suala hili tata.

Kambi ya wahafidhina ilitaka kupitisha mageuzi ya kikatiba ambayo yangetatiza maandalizi na kupitishwa kwa kura za maoni katika jimbo hili la kaskazini mwa nchi - na suala la uondoaji wa hiari wa ujauzito katika njia tofauti.

Haki za uavyaji mimba zitakuwa hatarini katika uchaguzi wa mwezi Novemba na Warepublican walitaka kufanya ushindi kwa kambi inayounga mkono uavyaji mimba kuwa ngumu zaidi. Lakini wapiga kura wa jimbo la Ohio wamepiga kura dhidi ya mageuzi hayo, kulingana na makadirio ya vyombo vya habari kutoka CNN na USA Today.

Ngome hii ya zamani ya tasnia ya Marekani, ambayo ilizua mshangao kwa kumpigia kura Donald Trump mnamo 2016, imetofautiana kwa suala la utoaji wa mimba tangu Mahakama ya Juu itoe nafasi kwa majimbo kutunga sheria juu ya swali hilo, mnamo mwezi Juni 2022.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.