Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Marekani: Donald Trump kufikishwa katika mahakama ya shirikisho Alhamisi hii

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump anashutumiwa kwa kujaribu kutumia mbinu za 'kihalifu' lililolenga kutengua matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameitwa katika mahakama ya shirikisho mjini Washington siku ya Alhamisi kujibu mashtaka yanayohusiana na mbinu zake za "kihalifu" kwa lengo la kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameitwa katika mahakama ya shirikisho mjini Washington siku ya Alhamisi kujibu mashtaka yanayohusiana na mbinu zake za "kihalifu" kwa lengo la kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020. © AFP - PATRICK T. FALLON
Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika kampeni ya kurejea tena katika ikulu ya White House, Donald Trump bado anapambana licha ya kesi nyingi mahakamani zinazomhusu. Rais huyo wa zamani wa Marekani ameitwa Alhamisi hii kwenye mahakama ya shirikisho mjini Washington kujibu mashtaka yanayohusiana na mbinu zake za "kihalifu" kwa lengo la kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Mashtaka ya kurasa 45 yaliyochapishwa Jumanne, ambayo yanataja "mpango mzima wa uhalifu", yanamtuhumu kwa kudhoofisha misingi ya demokrasia ya Marekani kwa kujaribu kubadilisha mchakato wa kuhesabu matokeo ya kura ya Wamarekani zaidi ya milioni 150, mashtaka ya kipekee na makubwa zaidi aliyoyafanya akiwa bado ni rais wa Marekani. Kwa upande mwingine, kesi mbili za awali za jinai zilizoletwa dhidi yake mwaka huu zinahusiana na kipindi cha kabla na baada ya muhula wake.

Mahakama ambayo inayo mashtaka yote dhidi yake inapatikana karibu na Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani, yaliyovamiwa na mamia ya wafuasi wake wenye msimamo mkali kuzuia kuthibitishwa kwa ushindi wa mpinzani wake Joe Biden, Januari 6, 2021.

Shambulio hili "lilitiwa moyo na uwongo" kuhusu madai ya udanganyifu katika uchaguzi kwa ajili ya Joe Biden uliofanywa kwa miezi kadhaa na mshtakiwa, amesema mwendesha mashtaka maalum Jack Smith, ambaye amesimamia uchunguzi, baada ya kuchapishwa kwa hati ya mashtaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.