Pata taarifa kuu

Mashirika ya haki za kiraia kupambana dhidi ya Donald Trump

Nchini Marekani, mashirika mawili ya yanayotetea haki za binadamu yanazindua wiki ya hatua dhidi ya Donald Trump. Wanatumai kumzuia rais huyo wa zamani kugombea nafasi yake kufuati kuhusika kwake katika shambulio la Capitol, kwa kutumia Katiba ya Marekani.

Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump anahudhuria hafla ya kampeni huko Council Bluffs, Iowa, Marekani, Julai 7, 2023.
Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump anahudhuria hafla ya kampeni huko Council Bluffs, Iowa, Marekani, Julai 7, 2023. © Scott Morgan / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu huko New York, Loubna Anaki

"Donald Trump ameshindwa" ndilo jina la kampeni iliyozinduliwa wiki hii na Mi familia Vota na Free Speech for the people, mashirika mawili ya kutetea haki za kiraia nchini Marekani.

Kwenye programu, maandamano katika majimbo kadhaa: California, Oregon na Georgia. Lakini juu ya yote, mashirika haya yanataka kuweka shinikizo kwa makatibu wa majimbo haya kumpiga marufuku Donald Trump kuwania katuka uchaguei. Kwa sababu makatibu wa Majimbo ndio wanahusikana jukumu la kuhalalisha ustahiki wa wagombea katika Majimbo yao.

Kwa upande wa mashirika yote mawili, yanasema Donald Trump hapaswi kuwa na haki ya kwania katika kiti cha urais. Yanatumai kuwa na uwezo wa kutumia marekebisho ya 14ᵉ ya Katiba kuunga mkono hatua yao. Katika nakala hii, marekebisho haya yanafanya kutostahiki mtu yeyote ambaye amekula kiapo cha kufikia Baraza la Congress, nafasi katika mahakama au serikali ya mtaa na ambaye aliiitisha uasi. Lakini Ibara hiyo haijataja ofisi ya rais.

Mi Familia Vota na Free Speech for the people wanatumai kuwa na uwezo wa kuwashawishi Makatibu wa Majimbo kuhusu tafsiri yao ya marekebisho ya 14ᵉ. Makundi haya mawili yanaamini kuwa Donald Trump alikiuka Katiba kwa kuwa na jukumu katika shambulio la Capitol.

Lakini hakuna uhakika kwamba juhudi zao zinatosha kumzuia Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.