Pata taarifa kuu

Marekani:Mshukiwa wa shambulio jimboni Tennessee alinunua bastola kihalali

NAIROBI – Polisi katika jimbo la Tennessee, nchini Marekani wamesema mshukiwa wa mauaji ya watu sita wakiwemo watoto watatu, waliokuwa Shuleni katika mji wa Nashville, alinunua bastola saba kihalali na kuzificha nyumbani.

Mtu aliyetekeleza shambulio katika mji wa Tennessee nchini Marekani alikuwa anamiliki bunduki kisheria
Mtu aliyetekeleza shambulio katika mji wa Tennessee nchini Marekani alikuwa anamiliki bunduki kisheria © AP/Jozen Reodica
Matangazo ya kibiashara

John Drake mkuu wa polisi katika mji huo pia amesema, mshukiwa huyo, wakati akitekeleza tukio hilo, alikuwa anapitia changamoto za kiakili.

"Alichukuliwa chini ya uangalizi kutokana na hali yake ya changamoto za hisia, maofisa wetu wamejulisha kuhusu matibabu aliyokuwa anapokea."ameeleza John Drake.

00:20

John Drake mkuu wa polisi katika mji wa Tennessee

Polisi wamezungumza na wazazi wa mshukiwa, Audrey Hale, ambaye aliuawa na polisi chini ya dakika 15 baada ya mashambulio hayo kuanza.

Hale, ambaye alijitambulisha kama mtu aliyebadili jinsia na aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, alikuwa amejihami kwa bunduki tatu, ikiwa ni pamoja na bunduki ya nusu-otomatiki.

Shambulio hilo lilitokea baada ya muuaji huyo kufanya ufuatiliaji wa eneo hilo, kuchora ramani na kuandika kile polisi walichokitaja kuwa ni "manifesto".

Wazazi wa Hale walidhani mshukiwa alikuwa na bunduki moja tu, lakini ilikuwa imeuzwa.

Waliamini mshukiwa "hapaswi kumiliki silaha", na hawakujua mshukiwa "alikuwa ameficha silaha kadhaa ndani ya nyumba", alisema Mkuu wa Polisi wa Nashville John Drake siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.