Nicaragua yawaachilia zaidi ya wafungwa 200 wa kisiasa wakiwemo wanawake wawili wa Ufaransa
Zaidi ya wafungwa 200 wa upinzani, wakiwemo wanawake wawili wa Ufaransa, wameachiliwa Alhamisi, Februari 9 huko Nicaragua na serikali ya Daniel Ortega na wako njiani kuelekea Marekani, ndugu na wapinzani walio uhamishoni wamesema.
Imechapishwa:
"Wafungwa 222 wa kisiasa wanawasili Washington, wameachiliwa huru," amesema katika video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii Arturo McFields, balozi wa zamani wa Nicaragua katika Umoja wa Mataifa ya Amerika (OAS), ambaye aliondolewa madarakani baada ya kuita nchi yake ya udikteta na ambaye sasa anaishi Marekani.
Javier Alvarez, raia wa Nicaragua anayeishi uhamishoni nchini Costa Rica, amelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba miongoni mwa walioachiliwa ni mke na binti yake, ambao pia wana uraia wa Ufaransa. Managua bado hajatoa taarifa yoyote rasmi.