Pata taarifa kuu
CHINA- MAREKANI- UHUSIANO

China yasikitishwa na hatua ya Marekani kudungua puto lake

Serikali ya China, hivi leo imeeleza kusikitishwa na kitendo cha jeshi la Marekani, kudungua puto lake inalosema liliingia kwa bahari mbaya katika anga ya Marekani, Washington ikidai lilikuwa linafanya udukuzi.

Marekani imedungua Puto la China
Marekani imedungua Puto la China REUTERS - RANDALL HILL
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza saa chache baada ya kudunguliwa kwa puto hilo, rais Joe Biden, amesisitiza kutofumbia macho vitendo vya uchokozi vya China.

“Siku ya Jumatano nipoaambiwa kuhusu hili puto niliamurisha jeshi kulitungua haraka iwezekanavyo.”ameeleza rais Joe Biden.

Hatua hii huenda ikazidisha mvutano zaidi kati ya nchi hizo mbili zenye nguvu duniani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.