Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Ghasia katika Bunge la Marekani: Warepublican washindwa kumchagua kiongozi wao

Mnamo 1856, ilichukua miezi 2 na duru 133 za upigaji kura kumteua Spika wa Baraza la Wawakilishi.

Ukumbi wa vikao vya Baraza la Wawakilishi katika makao makuu ya Baraza la Congress, Capitol, huko Washington, Feb. 28, 2022.
Ukumbi wa vikao vya Baraza la Wawakilishi katika makao makuu ya Baraza la Congress, Capitol, huko Washington, Feb. 28, 2022. AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Hili lilikuwa halijatokea kwa kipindi cha miaka 100: wajumbe waliochaguliwa wa Baraza la Wawakilishi la Marekani walimaliza kikao chao siku ya Jumanne bila kuwa na uwezo wa kumchagua spika, mvutano mkali katika safu ya Republican ulitumbukiza Baraza la Congress katika sintofahamu.

Aliyekuwa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Nancy Pelosi, Kevin McCarthy, mwenye umri wa miaka zaidi ya hamsini, hakuwa amefanikiwa baada ya upigaji kura mara tatu mfululizo kutuliza mjitengano uliotokana na kundi la wafuasi wa rais wa zamani Donald Trump wanaomchukulia kuwa mtu wa wastani kupita kiasi. Viongozi waliochaguliwa walikubali kusimamisha kura zao hadi Jumatano asubuhi.

Warepublikan, ambao walipata kura nyingi katika Baraza la Wawakilishi katika uchaguzi wa mwezi Novemba, walikuwa wameahidi kutumia nguvu zao mpya kwa kufungua msururu wa uchunguzi dhidi ya Rais wa Marekani Joe Biden.

Lakini malumbano ya ndani katika chama cha Republican ndio chanzo cha uhasama huo: wajumbe waliochaguliwa wa Baraza la Wawakilishi hawawezi kula kiapo rasmi, na hivyo kufungua uchunguzi wowote, wakati rais hajateuliwa.

Jumanne jioni Donald Trump alikosoa "msukosuko mkubwa" ndani ya chama ambapo anataka kupata uteuzi ili kutwaa tena Ikulu ya White House mnamo 2024.

Kiwango cha kura 218

Uchaguzi wa "spika", mtu wa tatu kwa umuhimu katika siasa za Marekani baada ya rais na makamu wa rais, unahitaji wingi wa kura, 218. Kizingiti ambacho Kevin McCarthy hangeweza kufikia, zaidi ya wabunge ishirini wanaomuunga mkono Donald Trump ndio walianzisha sintofahamu hiyo.

Ugombea wa Bw. McCarthy hata hivyo unaungwa mkono kwa kiasi kikubwa ndani ya chama chake: tangazo la uteuzi wake siku ya Jumanne katika makao makuu ya Baraza la Congress lilipokelewa kwa shangwe kubwa katika safu ya Republican.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.